‏ Numbers 15:5-12

5 aPamoja na kila mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa au dhabihu, andaa robo ya hini ya divai kwa sadaka ya kinywaji.

6 b“ ‘Pamoja na kondoo dume andaa sadaka ya nafaka ya sehemu mbili za kumi za efa
Sehemu mbili za kumi za efa ni sawa na kilo 2.
za unga laini uliochanganywa na theluthi moja
Theluthi moja ya hini ni sawa na lita moja na nusu.
ya hini ya mafuta,
7 ena theluthi moja ya hini ya divai kama sadaka ya kinywaji. Vitoe kama harufu nzuri inayompendeza Bwana.

8 f“ ‘Unapoandaa fahali mchanga kama sadaka ya kuteketezwa au dhabihu, kwa ajili ya nadhiri maalum au sadaka ya amani kwa Bwana, 9 gleta pamoja na huyo fahali sadaka ya nafaka ya unga laini sehemu tatu za kumi za efa
Sehemu tatu za kumi za efa ni sawa na kilo 3.
uliochanganywa na nusu ya hini
Nusu ya hini ni sawa na lita 2.
ya mafuta.
10 jPia utaleta nusu ya hini ya divai kama sadaka ya kinywaji. Itakuwa sadaka iliyoteketezwa kwa moto, harufu nzuri inayompendeza Bwana. 11Kila fahali au kondoo dume, kila mwana-kondoo au mbuzi mchanga, atatayarishwa kwa njia hii. 12 kFanyeni hivi kwa ajili ya kila mmoja, kwa kadiri ya wingi wa mtakavyoandaa.

Copyright information for SwhNEN