‏ Nahum 2:11-13


11 aLiko wapi sasa pango la simba,
mahali ambapo waliwalisha watoto wao,
ambapo simba dume na simba jike walikwenda
na ambapo wana simba walikwenda
bila kuogopa chochote?
12 bSimba aliua mawindo ya kutosha watoto wake,
alinyonga mawindo kwa ajili ya mwenzi wake,
akijaza makao yake kwa alivyoua
na mapango yake kwa mawindo.

13 c Bwana Mwenye Nguvu Zote anatangaza,
“Mimi ni kinyume na ninyi.
Magari yenu ya vita nitayateketeza kwa moto,
na upanga utakula wana simba wako.
Sitawaachia mawindo juu ya nchi.
Sauti za wajumbe wako
hazitasikika tena.”
Copyright information for SwhNEN