‏ Matthew 8:19-22

19 aKisha mwalimu mmoja wa sheria akamjia Yesu na kumwambia, “Mwalimu, nitakufuata kokote uendako.”

20 bNaye Yesu akamjibu, “Mbweha wana mapango, nao ndege wa angani wana viota, lakini Mwana wa Adamu hana mahali pa kulaza kichwa chake.”

21 cMwanafunzi mwingine akamwambia, “Bwana, niruhusu kwanza nikamzike baba yangu.”

22 dLakini Yesu akamwambia, “Nifuate, uwaache wafu wawazike wafu wao.”

Copyright information for SwhNEN