Matthew 27:57-61
Maziko Ya Yesu
(Marko 15:42-47; Luka 23:50-56; Yohana 19:38-42)
57 aIlipofika jioni, alifika mtu mmoja tajiri kutoka Arimathaya aitwaye Yosefu, ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu. 58Akamwendea Pilato ili kumwomba mwili wa Yesu. Pilato akaamuru apewe. 59Yosefu akauchukua mwili wa Yesu, akaufunga katika kitambaa cha kitani safi, 60 bna kuuweka katika kaburi lake mwenyewe jipya, alilokuwa amelichonga kwenye mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa katika ingilio la kaburi, akaenda zake. 61Maria Magdalene na yule Maria mwingine walikuwepo mahali pale, wakiwa wameketi mkabala na kaburi.
Copyright information for
SwhNEN