Matthew 27:3-10
Yuda Ajinyonga
(Matendo 1:18-19)
3 aYuda, ambaye alikuwa amemsaliti Yesu, alipoona kuwa Yesu amehukumiwa, akajuta na akarudisha vile vipande thelathini vya fedha alivyopewa na viongozi wa makuhani na wazee wa watu. 4 bAkasema, “Nimetenda dhambi, kwa maana nimeisaliti damu isiyo na hatia.”Wakamjibu, “Hilo latuhusu nini sisi? Ni shauri yako.”
5 cBasi Yuda akavitupa vile vipande vya fedha ndani ya Hekalu akaondoka akaenda kujinyonga.
6 dWale viongozi wa makuhani wakazichukua zile fedha wakasema, “Si halali kuchanganya fedha hizi na sadaka kwa sababu hizi ni fedha zenye damu.” 7Kwa hiyo baada ya kushauriana, waliamua kuzitumia kununulia shamba la mfinyanzi, liwe mahali pa kuzikia wageni. 8 eHii ndiyo sababu lile shamba likaitwa Shamba la Damu hadi leo. 9 fNdipo likatimia lile lililonenwa na nabii Yeremia, kwamba, “Walichukua vile vipande thelathini vya fedha, thamani aliyopangiwa na watu wa Israeli, 10 gwakanunulia shamba la mfinyanzi, kama vile Bwana alivyoniagiza.”
Copyright information for
SwhNEN