‏ Matthew 27:27-31

Askari Wamdhihaki Yesu

(Marko 15:16-20; Yohana 19:2-3)

27 aKisha askari wa mtawala wakampeleka Yesu kwenye Praitorio
Praitorio maana yake ni makao makuu ya mtawala, jumba la kifalme lililokuwa linakaliwa na Pontio Pilato huko Yerusalemu, palipokuwa na kiti cha hukumu.
na wakakusanya kikosi kizima cha askari kumzunguka.
28 cWakamvua nguo zake na kumvika vazi la rangi nyekundu, kisha 29 dwakasokota taji ya miiba, wakaiweka kichwani pake. Wakamwekea fimbo katika mkono wake wa kuume, na wakapiga magoti mbele zake na kumdhihaki, wakisema, “Salamu, mfalme wa Wayahudi!” 30 eWakamtemea mate, wakachukua ile fimbo wakampiga kichwani tena na tena. 31 fBaada ya kumdhihaki, wakamvua lile joho, wakamvika tena nguo zake. Kisha wakampeleka ili wakamsulubishe.

Copyright information for SwhNEN