‏ Matthew 26:6-13

Yesu Anapakwa Mafuta Huko Bethania

(Marko 14:3-9; Yohana 12:1-8)

6 aYesu alikuwa Bethania nyumbani mwa Simoni aliyekuwa na ukoma, 7naye mwanamke mmoja akamjia akiwa na chupa ya marhamu yenye manukato ya thamani kubwa; akayamimina kichwani mwa Yesu alipokuwa ameketi mezani kula chakula.

8 bLakini wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, “Upotevu huu wote ni wa nini? 9Manukato haya yangeuzwa kwa bei kubwa, na fedha hizo wakapewa maskini.”

10 cYesu, akijua jambo hili, akawaambia, “Mbona mnamsumbua huyu mwanamke? Yeye amenitendea jambo zuri sana. 11 dMaskini mtakuwa nao siku zote, lakini mimi hamtakuwa nami siku zote. 12 eAlipomiminia haya manukato kwenye mwili wangu, amefanya hivyo ili kuniandaa kwa ajili ya maziko yangu. 13Amin, nawaambia, mahali popote ulimwenguni ambapo hii Injili itahubiriwa, jambo hili alilolitenda huyu mwanamke litatajwa pia kwa ukumbusho wake.”

Copyright information for SwhNEN