Matthew 26:57-68
Yesu Mbele Ya Kuhani Mkuu
(Marko 14:53-65; Luka 22:54-71; Yohana 18:13-24)
57 aWale waliokuwa wamemkamata Yesu wakampeleka kwa Kayafa, kuhani mkuu, mahali ambapo walimu wa sheria pamoja na wazee walikuwa wamekusanyika. 58 bLakini Petro akamfuata kwa mbali hadi uani kwa kuhani mkuu. Akaingia ndani, akaketi pamoja na walinzi ili aone litakalotukia.59 cViongozi wa makuhani na Baraza la Wayahudi lote wakatafuta ushahidi wa uongo dhidi ya Yesu ili wapate kumuua. 60 dLakini hawakupata jambo lolote, ingawa mashahidi wengi wa uongo walijitokeza.
Hatimaye wakajitokeza mashahidi wawili wa uongo 61 ena kusema, “Huyu mtu alisema, ‘Ninaweza kulivunja Hekalu la Mungu na kulijenga tena kwa siku tatu.’ ”
62 fKisha kuhani mkuu akasimama na kumwambia Yesu, “Je, wewe hutajibu? Ni ushahidi gani hawa watu wanauleta dhidi yako?” 63 gLakini Yesu akakaa kimya.
Ndipo kuhani mkuu akamwambia, “Nakuapisha mbele za Mungu aliye hai. Tuambie kama wewe ndiwe Kristo, ▼
▼Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
Mwana wa Mungu.”64 iYesu akajibu, “Wewe umenena. Lakini ninawaambia nyote: Siku za baadaye, mtamwona Mwana wa Adamu akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mwenye Nguvu, na akija juu ya mawingu ya mbinguni.”
65 jNdipo kuhani mkuu akararua mavazi yake na kusema, “Amekufuru! Tuna haja gani tena ya mashahidi zaidi? Tazama, sasa ninyi mmesikia hayo makufuru. 66 kUamuzi wenu ni gani?”
Wakajibu, “Anastahili kufa.”
67 lKisha wakamtemea mate usoni na wengine wakampiga ngumi. Wengine wakampiga makofi 68 mna kusema, “Tutabirie, wewe Kristo! Ni nani aliyekupiga?”
Copyright information for
SwhNEN