Matthew 26:31-35
Yesu Atabiri Petro Kumkana
(Marko 14:27-31; Luka 22:31-34; Yohana 13:36-38)
31 aKisha Yesu akawaambia, “Usiku huu, ninyi nyote mtaniacha, kwa maana imeandikwa:“ ‘Nitampiga mchungaji,
nao kondoo wa hilo kundi watatawanyika.’
32 b Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya.”
33Petro akajibu, “Hata kama wote watakuacha, kamwe mimi sitakuacha.”
34 cYesu akamjibu, “Amin, nakuambia, usiku huu, kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.”
35 dLakini Petro akasisitiza, “Hata kama itabidi kufa pamoja nawe, sitakukana kamwe.” Nao wanafunzi wale wengine wote wakasema vivyo hivyo.
Copyright information for
SwhNEN