Matthew 24:45-47
Mfano Wa Mtumishi Mwaminifu
(Luka 12:41-48)
45 a “Ni nani basi aliye mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake amemweka kusimamia watumishi wengine katika nyumba yake, ili awape chakula chao kwa wakati unaofaa? 46 bHeri mtumishi yule ambaye bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo. 47 cAmin, nawaambia, atamweka mtumishi huyo kuwa msimamizi wa mali yake yote.
Copyright information for
SwhNEN