‏ Matthew 22:7-19

7 aYule mfalme akakasirika sana, akapeleka jeshi lake likawaangamiza wale wauaji na kuuteketeza mji wao kwa moto.

8 b “Kisha akawaambia watumishi wake, ‘Karamu ya arusi imeshakuwa tayari, lakini wale niliowaalika hawakustahili kuja. 9 cKwa hiyo nendeni katika njia panda mkamwalike karamuni yeyote mtakayemwona.’ 10 dWale watumishi wakaenda barabarani, wakawakusanya watu wote waliowaona, wema na wabaya. Ukumbi wa arusi ukajaa wageni.

11 e “Lakini mfalme alipoingia ndani ili kuwaona wageni, akamwona mle mtu mmoja ambaye hakuwa amevaa vazi la arusi. 12 fMfalme akamuuliza, ‘Rafiki, uliingiaje humu bila vazi la arusi?’ Yule mtu hakuwa na la kusema.

13 g “Ndipo mfalme akawaambia watumishi wake, ‘Mfungeni mikono na miguu mkamtupe nje, kwenye giza. Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.’

14 h “Kwa maana walioitwa ni wengi, lakini walioteuliwa ni wachache.”

Kulipa Kodi Kwa Kaisari

(Marko 12:13-17; Luka 20:20-26)

15 iNdipo Mafarisayo wakatoka nje wakaandaa mpango wa kumtega Yesu katika maneno yake. 16 jWakatuma wanafunzi wao kwake pamoja na Maherode. Nao wakasema, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwadilifu na unafundisha njia ya Mungu katika kweli bila kuyumbishwa na mtu wala kuonyesha upendeleo. 17 kTuambie basi, wewe unaonaje? Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la?”

18Lakini Yesu, akijua makusudi yao mabaya, akawaambia, “Enyi wanafiki, kwa nini mnajaribu kunitega? 19Nionyesheni hiyo sarafu inayotumika kwa kulipia kodi.” Wakamletea dinari.
Copyright information for SwhNEN