‏ Matthew 22:41-46

Swali Kuhusu Mwana Wa Daudi

(Marko 12:35-37; Luka 20:41-44)

41 aWakati Mafarisayo walikuwa wamekusanyika pamoja, Yesu akawauliza, 42 b“Mnaonaje kuhusu Kristo?
Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
Yeye ni mwana wa nani?”

Wakamjibu, “Yeye ni mwana wa Daudi.”

43Akawaambia, “Inakuwaje basi kwamba Daudi, akinena kwa kuongozwa na Roho, anamwita Kristo ‘Bwana’? Kwa maana asema,

44 d “ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu:
“Keti mkono wangu wa kuume,
hadi nitakapowaweka adui zako
chini ya miguu yako.” ’
45 Kama basi Daudi anamwita yeye ‘Bwana,’ awezaje kuwa mwanawe?” 46 eHakuna mtu aliyeweza kumjibu Yesu neno. Tena tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu kumuuliza tena maswali.

Copyright information for SwhNEN