‏ Matthew 21:1-11

Yesu Anaingia Yerusalemu Kwa Shangwe

(Marko 11:1-11; Luka 19:28-40; Yohana 12:12-19)

1 aWalipokaribia Yerusalemu, wakafika Bethfage katika Mlima wa Mizeituni. Ndipo Yesu akawatuma wanafunzi wake wawili, 2akawaambia, “Nendeni katika kijiji kilichoko mbele yenu, nanyi mtamkuta punda amefungwa hapo, na mwana-punda pamoja naye. Wafungueni na mniletee. 3 bKama mtu yeyote akiwasemesha lolote, mwambieni kwamba Bwana ana haja nao, naye atawaruhusu mwalete mara.”

4 cHaya yalitukia ili litimie lile lililonenwa na nabii, akisema:

5 d“Mwambieni Binti Sayuni,
‘Tazama, mfalme wako anakuja kwako,
ni mnyenyekevu, naye amepanda punda,
juu ya mwana-punda, mtoto wa punda.’ ”
6 eWale wanafunzi wakaenda, wakafanya kama Yesu alivyokuwa amewaagiza. 7 fWakamleta yule punda na mwana-punda, nao wakatandika mavazi yao juu ya hao punda, naye Yesu akaketi juu yake. 8 gUmati mkubwa wa watu ukatandaza mavazi yao barabarani, na wengine wakakata matawi kutoka kwenye miti, wakayatandaza barabarani. 9 hUle umati wa watu uliomtangulia na ule uliomfuata ukapiga kelele ukisema,

“Hosana,
Kiebrania kusema Okoa, basi likawa neno la shangwe.
Mwana wa Daudi!”

“Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!”

“Hosana juu mbinguni!”
10 jYesu alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakauliza, “Huyu ni nani?”

11 kUle umati wa watu ukajibu, “Huyu ni Yesu, yule nabii kutoka Nazareti katika Galilaya.”


Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.

Everyone uses cookies. We do too! Cookies are little bits of information stored on your computer which help us give you a better experience. You can find out more by reading the STEPBible cookie policy.