Matthew 16:13-19
Petro Amkiri Yesu Kuwa Ni Mwana Wa Mungu
(Marko 8:27-30; Luka 9:18-21)
13 aBasi Yesu alipofika katika eneo la Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake, “Watu husema kwamba mimi Mwana wa Adamu ni nani?”14 bWakamjibu, “Baadhi husema ni Yohana Mbatizaji; wengine husema ni Eliya; na bado wengine husema ni Yeremia au mmojawapo wa manabii.”
15Akawauliza, “Je, ninyi mnasema mimi ni nani?”
16 cSimoni Petro akamjibu, “Wewe ndiwe Kristo, ▼
▼Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
Mwana wa Mungu aliye hai.” 17 eNaye Yesu akamwambia, “Heri wewe, Simoni Bar-Yona, ▼
▼Bar-Yona ni neno la Kiaramu, maana yake ni Mwana wa Yona.
kwa maana hili halikufunuliwa kwako na mwanadamu, bali na Baba yangu aliye mbinguni. 18 gNami nakuambia, wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, hata malango ya Kuzimu hayataweza kulishinda. 19 hNitakupa funguo za Ufalme wa mbinguni, na lolote utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa Mbinguni, nalo lolote utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.”
Copyright information for
SwhNEN