‏ Matthew 14:17-21

17 aWakamjibu, “Tuna mikate mitano na samaki wawili tu.”

18Akawaambia, “Nileteeni hivyo vitu hapa.” 19 bYesu akaagiza makutano wakae chini kwenye nyasi. Akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi, nao wanafunzi wakawagawia makutano. 20 cWote wakala, wakashiba. Nao wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu kumi na viwili. 21Idadi ya watu waliokula walikuwa wanaume wapatao 5,000, bila kuhesabu wanawake na watoto.

Copyright information for SwhNEN