Mark 8:27-29
Petro Amkiri Yesu Kuwa Ndiye Kristo
(Mathayo 16:13-20; Luka 9:18-21)
27 aYesu na wanafunzi wake wakaondoka kwenda katika vijiji vya Kaisaria-Filipi. Walipokuwa njiani, Yesu akawauliza, “Watu husema mimi ni nani?”28 bWakamjibu, “Baadhi husema wewe ni Yohana Mbatizaji, wengine husema ni Eliya, na bado wengine husema wewe ni mmojawapo wa manabii.”
29 cAkawauliza, “Je, ninyi mnasema mimi ni nani?”
Petro akajibu, “Wewe ndiwe Kristo.” ▼
▼Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
Copyright information for
SwhNEN