‏ Mark 3:31-35

Mama Na Ndugu Zake Yesu

(Mathayo 12:46-50; Luka 8:19-21)

31 aKisha wakaja ndugu zake Yesu pamoja na mama yake. Wakasimama nje, wakamtuma mtu kumwita. 32Umati wa watu ulikuwa umeketi kumzunguka, nao wakamwambia, “Mama yako na ndugu zako wako nje, wanakutafuta.”

33Akawauliza, “Mama yangu na ndugu zangu ni nani?”

34Kisha akawatazama wale watu waliokuwa wameketi kumzunguka pande zote, akasema, “Hawa ndio mama yangu na ndugu zangu. 35Mtu yeyote anayetenda mapenzi ya Mungu, huyo ndiye ndugu yangu, na dada yangu na mama yangu.”

Copyright information for SwhNEN