‏ Mark 3:13-19

Yesu Achagua Mitume Kumi Na Wawili

(Mathayo 10:1-4; Luka 6:12-16)

13 aYesu akapanda mlimani na kuwaita wale aliowataka, nao wakamjia. 14 bAkawachagua kumi na wawili, ambao aliwaita mitume, ili wapate kuwa pamoja naye, na awatume kwenda kuhubiri 15 cna kuwa na mamlaka ya kutoa pepo wachafu. 16 dHawa ndio wale kumi na wawili aliowachagua: Simoni (ambaye alimwita Petro); 17 eYakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye (ambao aliwaita Boanerge, maana yake Wana wa Ngurumo); 18Andrea, Filipo, Bartholomayo, Mathayo, Tomaso, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkananayo, 19na Yuda Iskariote aliyemsaliti Yesu.


Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.

Everyone uses cookies. We do too! Cookies are little bits of information stored on your computer which help us give you a better experience. You can find out more by reading the STEPBible cookie policy.