‏ Mark 16:9-11

Yesu Anamtokea Maria Magdalene

(Mathayo 28:9-10; Yohana 20:11-18)

9 aYesu alipofufuka alfajiri na mapema siku ya kwanza ya juma alimtokea kwanza Maria Magdalene, yule ambaye alikuwa amemtoa pepo wachafu saba. 10 bMaria akaenda, naye akawaambia wale waliokuwa wamefuatana na Yesu, waliokuwa wanaomboleza na kulia. 11 cLakini waliposikia kwamba Yesu yu hai na kwamba Maria alikuwa amemwona, hawakusadiki.

Copyright information for SwhNEN