Mark 15:1-5
Yesu Mbele Ya Pilato
(Mathayo 27:1-14; Luka 23:1-5; Yohana 18:28-38)
1 aAsubuhi na mapema, viongozi wa makuhani, pamoja na wazee, walimu wa sheria na Baraza lote, wakafikia uamuzi. Wakamfunga Yesu, wakamchukua na kumkabidhi kwa Pilato.2 bPilato akamuuliza, “Je, wewe ndiye Mfalme wa Wayahudi?”
Yesu akajibu, “Wewe umesema.”
3Viongozi wa makuhani wakamshtaki kwa mambo mengi. 4 cPilato akamuuliza tena, “Je, huna la kujibu? Tazama ni mashtaka mangapi wanayaleta juu yako.”
5 dLakini Yesu hakujibu lolote, hivyo Pilato akashangaa.
Copyright information for
SwhNEN