‏ Mark 13:14-19

Chukizo La Uharibifu

(Mathayo 24:15-28; Luka 21:20-24)

14 a “Mtakapoona ‘chukizo la uharibifu’ limesimama mahali pasipolipasa (asomaye na afahamu), basi wale walioko Uyahudi wakimbilie milimani. 15Yeyote aliye juu ya dari ya nyumba asishuke au kuingia ndani ili kuchukua chochote. 16Aliye shambani asirudi nyumbani kuchukua vazi lake. 17 bOle wao wenye mimba na wale wanaonyonyesha watoto siku hizo! 18Ombeni mambo haya yasitokee wakati wa baridi. 19 cKwa maana siku hizo zitakuwa za dhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo, hapo Mungu alipoumba ulimwengu, mpaka leo, na wala haitakuwako tena kamwe.
Copyright information for SwhNEN