Mark 11:15-19
Yesu Atakasa Hekalu
(Mathayo 21:12-17; Luka 19:45-48; Yohana 2:13-22)
15 aWalipofika Yerusalemu, Yesu akaingia katika eneo la Hekalu, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakinunua na kuuza humo ndani. Akazipindua meza za wale waliokuwa wakibadilisha fedha, na pia viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa, 16wala hakumruhusu mtu yeyote kuchukua bidhaa kupitia ukumbi wa Hekalu. 17 bNaye alipokuwa akiwafundisha, akasema, “Je, haikuandikwa kuwa:“ ‘Nyumba yangu itaitwa
nyumba ya sala kwa mataifa yote’?
Lakini ninyi mmeifanya kuwa ‘pango la wanyangʼanyi.’ ”
18 cViongozi wa makuhani na walimu wa sheria wakapata habari hizi, nao wakaanza kutafuta njia ya kumuua, kwa kuwa walikuwa wakimwogopa, kwa sababu umati wote ulikuwa unashangazwa na mafundisho yake.
19 dIlipofika jioni, Yesu na wanafunzi wake wakatoka nje ya mji.
Copyright information for
SwhNEN