‏ Mark 1:16-20

Yesu Awaita Wanafunzi Wanne

(Mathayo 4:12-22; Luka 4:14-15; 5:1-11)

16 aYesu alipokuwa akitembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona Simoni na Andrea nduguye wakizitupa nyavu zao baharini, kwa kuwa wao walikuwa wavuvi. 17 bYesu akawaambia, “Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu.” 18 cMara wakaacha nyavu zao, wakamfuata.

19 dAlipokwenda mbele kidogo, akamwona Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana nduguye, wakiwa kwenye mashua yao wakizitengeneza nyavu zao. 20Papo hapo akawaita, nao wakamwacha Zebedayo baba yao kwenye mashua pamoja na watumishi wa kuajiriwa, nao wakamfuata Yesu.


Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.