‏ Luke 9:1-6

Yesu Awatuma Wale Kumi Na Wawili

(Mathayo 10:5-15; Marko 6:7-13)

1 aYesu kisha akawaita wale kumi na wawili pamoja, akawapa mamlaka na uwezo wa kutoa pepo wachafu wote na kuponya magonjwa yote, 2 bkisha akawatuma waende wakahubiri Ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa. 3 cAkawaagiza akisema, “Msichukue chochote safarini: sio fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, hata msichukue kanzu ya ziada. 4 dKatika nyumba yoyote mwingiayo, kaeni humo hadi mtakapoondoka katika mji huo. 5 eKama watu wasipowakaribisha, mnapoondoka katika mji wao, kungʼuteni mavumbi kutoka kwenye miguu yenu ili kuwa ushuhuda dhidi yao.” 6 fHivyo wale wanafunzi wakaondoka wakaenda kutoka kijiji hadi kijiji, wakihubiri habari njema na kuponya wagonjwa kila mahali.

Copyright information for SwhNEN