‏ Luke 9:1-20

Yesu Awatuma Wale Kumi Na Wawili

(Mathayo 10:5-15; Marko 6:7-13)

1 aYesu kisha akawaita wale kumi na wawili pamoja, akawapa mamlaka na uwezo wa kutoa pepo wachafu wote na kuponya magonjwa yote, 2 bkisha akawatuma waende wakahubiri Ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa. 3 cAkawaagiza akisema, “Msichukue chochote safarini: sio fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, hata msichukue kanzu ya ziada. 4 dKatika nyumba yoyote mwingiayo, kaeni humo hadi mtakapoondoka katika mji huo. 5 eKama watu wasipowakaribisha, mnapoondoka katika mji wao, kungʼuteni mavumbi kutoka kwenye miguu yenu ili kuwa ushuhuda dhidi yao.” 6 fHivyo wale wanafunzi wakaondoka wakaenda kutoka kijiji hadi kijiji, wakihubiri habari njema na kuponya wagonjwa kila mahali.

Herode Afadhaika

(Mathayo 14:1-12; Marko 6:14-29)

7 gBasi Mfalme Herode, mtawala wa Galilaya, alisikia habari za yote yaliyotendeka. Naye akafadhaika, kwa kuwa baadhi ya watu walikuwa wakisema Yohana Mbatizaji amefufuliwa kutoka kwa wafu. 8 hWengine wakasema Eliya amewatokea, na wengine wakasema kwamba mmoja wa manabii wa kale amefufuka. 9 iHerode akasema, “Yohana nilimkata kichwa. Lakini ni nani huyu ambaye ninasikia mambo kama haya kumhusu?” Akatamani sana kumwona.

Yesu Awalisha Wanaume 5,000

(Mathayo 14:13-21; Marko 6:30-44; Yohana 6:1-14)

10 jMitume wake waliporudi, wakamweleza Yesu yote waliyofanya. Akawachukua, akaenda nao faraghani mpaka mji uitwao Bethsaida. 11 kLakini umati wa watu ukafahamu alikokwenda, ukamfuata. Akawakaribisha na kunena nao kuhusu Ufalme wa Mungu na kuwaponya wale wote waliokuwa wanahitaji uponyaji.

12 lIlipokaribia jioni, wale mitume kumi na wawili wakaenda kwa Yesu na kumwambia, “Waage makutano ili waende vijijini jirani na mashambani, ili wapate chakula na mahali pa kulala, kwa maana hapa tuko nyikani.”

13Yesu akawajibu, “Ninyi wapeni chakula.”

Nao wakajibu, “Hatuna zaidi ya mikate mitano na samaki wawili. Labda twende tukanunue chakula cha kuwatosha watu hawa wote.”
14Walikuwako wanaume wapatao 5,000.

Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Waketisheni katika makundi ya watu hamsini hamsini.”
15Wanafunzi wakafanya hivyo, wakawaketisha wote. 16 mYesu akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni, akavibariki na kuvimega. Kisha akawapa wanafunzi ili wawagawie watu. 17Wote wakala, wakashiba. Nao wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu kumi na viwili.

Petro Amkiri Yesu Kuwa Ndiye Kristo

(Mathayo 16:13-19; Marko 8:27-29)

18 nWakati mmoja, Yesu alipokuwa akiomba faraghani, nao wanafunzi wake wakiwa pamoja naye, akawauliza, “Watu husema mimi ni nani?”

19 oWakamjibu, “Baadhi husema wewe ni Yohana Mbatizaji, wengine husema ni Eliya, na bado wengine husema kwamba ni mmoja wa manabii wa kale amefufuka kutoka kwa wafu.”

20 pKisha akawauliza, “Je, ninyi mnasema mimi ni nani?”

Petro akajibu, “Wewe ndiwe Kristo
Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
wa Mungu.”

Copyright information for SwhNEN