‏ Luke 3:3-21

3 aAkaenda katika nchi yote kandokando ya Mto Yordani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi. 4 bKama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya:

“Sauti ya mtu aliaye nyikani,
‘Itengenezeni njia ya Bwana,
yanyoosheni mapito yake.
5Kila bonde litajazwa,
kila mlima na kilima vitashushwa.
Njia zilizopinda zitanyooshwa,
na zilizoparuza zitasawazishwa.
6 cNao watu wote watauona
wokovu wa Mungu.’ ”
7 dYohana akauambia ule umati wa watu uliokuwa unakuja ili kubatizwa naye, “Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu inayokuja? 8 eBasi zaeni matunda yastahiliyo toba. Wala msianze kusema mioyoni mwenu kuwa, ‘Sisi tunaye Abrahamu, baba yetu.’ Kwa maana nawaambia kuwa Mungu anaweza kumwinulia Abrahamu watoto kutoka mawe haya. 9 fHata sasa shoka limeshawekwa tayari kwenye shina la kila mti. Basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.”

10 gUle umati wa watu ukamuuliza, “Inatupasa tufanyeje basi?”

11 hYohana akawaambia, “Aliye na kanzu mbili amgawie asiye nayo, naye aliye na chakula na afanye vivyo hivyo.”

12 iWatoza ushuru nao wakaja ili wabatizwe, wakamuuliza, “Bwana na sisi inatupasa tufanyeje?”

13 jAkawaambia, “Msichukue zaidi ya kiwango mlichopangiwa.”

14 kAskari nao wakamuuliza, “Je, nasi inatupasa tufanye nini?”

Akawaambia, “Msimdhulumu mtu wala msimshtaki mtu kwa uongo, bali mridhike na mishahara yenu.”

15 lWatu walikuwa na matazamio makubwa. Wakawa wanajiuliza mioyoni mwao iwapo Yohana angeweza kuwa ndiye Kristo.
Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
16 nYohana akawajibu akawaambia, “Mimi nawabatiza kwa maji.
Tafsiri nyingine zinasema ndani ya maji.
Lakini atakuja aliye na nguvu kuniliko mimi, ambaye sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
17 pPepeto lake liko mkononi, tayari kusafisha sakafu yake ya kupuria na kuikusanya ngano ghalani, lakini makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.” 18Basi, kwa maonyo mengine mengi Yohana aliwasihi na kuwahubiria watu Habari Njema.

19 qLakini Yohana alipomkemea Mfalme Herode kuhusu uhusiano wake na Herodia, mke wa ndugu yake, na maovu mengine aliyokuwa amefanya, 20 rHerode aliongezea jambo hili kwa hayo mengine yote: alimfunga Yohana gerezani.

Kubatizwa Kwa Bwana Yesu

(Mathayo 3:13-17; Marko 1:9-11)

21 sBaada ya watu wote kubatizwa, Yesu naye akabatizwa. Naye alipokuwa akiomba, mbingu zilifunguka.
Copyright information for SwhNEN