‏ Luke 24:50-53

Kupaa Kwa Yesu Mbinguni

(Marko 16:19-20; Matendo 1:9-11)

50 aAkiisha kuwaongoza mpaka kwenye viunga vya Bethania, akainua mikono yake juu na kuwabariki. 51 bAlipokuwa anawabariki, akawaacha, akachukuliwa mbinguni. 52 cKisha wakamwabudu na kurudi Yerusalemu wakiwa wamejawa na furaha kuu. 53 dNao wakadumu ndani ya Hekalu wakimtukuza Mungu. Amen.

Copyright information for SwhNEN