‏ Luke 24:39-43

39 aTazameni mikono yangu na miguu yangu, mwone kuwa ni mimi hasa. Niguseni mwone; kwa maana mzuka hauna nyama na mifupa, kama mnionavyo kuwa navyo.”

40Aliposema haya, akawaonyesha mikono na miguu yake. 41 bWakashindwa kuamini kwa ajili ya furaha na mshangao waliokuwa nao. Akawauliza, “Mna chakula chochote hapa?”

42Wakampa kipande cha samaki aliyeokwa, 43 cnaye akakichukua na kukila mbele yao.

Copyright information for SwhNEN