‏ Luke 23:1-5

Yesu Apelekwa Kwa Pilato

(Mathayo 27:1-14; Marko 15:1-5; Yohana 18:28-38)

1 aKisha umati wote wa watu ukainuka na kumpeleka Yesu kwa Pilato. 2 bNao wakaanza kumshtaki wakisema: “Tumemwona huyu mtu akipotosha taifa letu, akiwazuia watu wasilipe kodi kwa Kaisari na kujiita kuwa yeye ni Kristo,
Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
mfalme.”

3 dBasi Pilato akamuuliza Yesu, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?”

Yesu akajibu, “Wewe wasema.”

4 ePilato akawaambia viongozi wa makuhani na watu wote waliokuwepo, “Sioni sababu ya kutosha kumshtaki mtu huyu!”

5 fLakini wao wakakazana kusema, “Anawachochea watu kwa mafundisho yake katika Uyahudi yote, tangu Galilaya alikoanzia, hadi sehemu hii!”


Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.