Luke 22:31-34
Yesu Atabiri Kuwa Petro Atamkana
31 aYesu akasema, “Simoni, Simoni, sikiliza, Shetani ameomba kuwapepeta ninyi wote kama ngano. 32 bLakini nimekuombea wewe Simoni ili imani yako isishindwe, nawe ukiisha kunirudia, uwaimarishe ndugu zako.”33 cPetro akajibu, “Bwana, niko tayari kwenda pamoja nawe gerezani na hata kifoni.”
34 dYesu akamjibu, “Ninakuambia Petro, kabla jogoo hajawika usiku wa leo, utakana mara tatu kwamba hunijui mimi.”
Copyright information for
SwhNEN