‏ Luke 21:20-24

Kuharibiwa Kwa Yerusalemu Kwatabiriwa

(Mathayo 24:15-21; Marko 13:14-19)

20 a “Mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, basi fahamuni kwamba kuharibiwa kwake kumekaribia. 21 bWakati huo, wale walio Uyahudi wakimbilie milimani, walio mjini Yerusalemu watoke humo, nao wale walioko mashambani wasiingie mjini. 22 cKwa sababu huu utakuwa ni wakati wa adhabu ili kutimiza yote yaliyoandikwa. 23 dOle wao wenye mimba na wale wanaonyonyesha watoto siku hizo! Kutakuwa na dhiki kuu katika nchi na ghadhabu juu ya hawa watu. 24 eWataanguka kwa makali ya upanga, na wengine watachukuliwa kuwa mateka katika mataifa yote. Nao mji wa Yerusalemu utakanyagwa na watu wa Mataifa hadi muda wa hao watu wa Mataifa utimie.

Copyright information for SwhNEN