Luke 20:45-47
Yesu Awashutumu Walimu Wa Sheria
(Mathayo 23:1-36; Marko 12:38-40)
45 aWakati watu wote walikuwa wanamsikiliza, Yesu akawaambia wanafunzi wake, 46 b“Jihadharini na walimu wa sheria. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa kwa heshima masokoni. Hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi, na kukaa kwenye nafasi za heshima katika karamu. 47 cWao hula nyumba za wajane, na ili waonekane kuwa wema, wanasali sala ndefu. Watu kama hawa watapata hukumu iliyo kuu sana.”
Copyright information for
SwhNEN