Luke 18:9-12
Mfano Wa Farisayo Na Mtoza Ushuru
9 aYesu akatoa mfano huu kwa wale waliojiamini kuwa wao ni wenye haki na kuwadharau wengine: 10 b“Watu wawili walikwenda Hekaluni kusali, mmoja wao alikuwa Farisayo na mwingine alikuwa mtoza ushuru. 11 cYule Farisayo, akasimama, akasali hivi na kuomba kwake mwenyewe: ‘Mungu, nakushukuru kwa sababu mimi si kama watu wengine ambao ni wanyangʼanyi, wadhalimu, na wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. 12 dMimi nafunga mara mbili kwa juma, na natoa sehemu ya kumi ya mapato yangu.’
Copyright information for
SwhNEN