Leviticus 6:20-23
20 a“Hii ni sadaka ambayo Aroni na wanawe wanapaswa kuleta kwa Bwana siku atakapotiwa mafuta: sehemu ya kumi ya efa ▼▼Sehemu ya kumi ya efa ni sawa na kilo moja.
ya unga laini kama sadaka ya kawaida ya nafaka. Nusu yake ataitoa asubuhi na nusu nyingine jioni. 21 cIandae kwa mafuta kwenye kikaango; ilete ikiwa imechanganywa vizuri, na utoe hiyo sadaka ya nafaka ikiwa imevunjwa vipande vipande kuwa harufu nzuri ya kumpendeza Bwana. 22Mwanawe atakayeingia mahali pake kama kuhani aliyetiwa mafuta ndiye atakayeiandaa. Ni fungu la kawaida la Bwana, nalo litateketezwa kabisa. 23Kila sadaka ya nafaka ya kuhani itateketezwa kabisa; kamwe haitaliwa.”
Copyright information for
SwhNEN