Leviticus 24:2-6
2 a“Waagize Waisraeli wakuletee mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa kwa ajili ya mwanga ili taa ziwe zinawaka daima. 3 bNje ya pazia la Ushuhuda ndani ya Hema la Kukutania, Aroni ataziwasha taa mbele za Bwana kuanzia jioni hadi asubuhi bila kuzima. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo. 4 cTaa zilizo juu ya kinara cha dhahabu safi mbele za Bwana lazima zihudumiwe daima.5 d“Chukua unga laini, uoke mikate kumi na miwili, ukitumia sehemu mbili za kumi za efa ▼
▼Sehemu mbili za kumi za efa ni sawa na kilo mbili.
za unga kwa kila mkate. 6 fIweke katika mistari miwili, kila mstari mikate sita, uiweke mbele za Bwana juu ya meza iliyotengenezwa kwa dhahabu safi.
Copyright information for
SwhNEN