a Kut 6:23; 24:1; 28:1; 30:9; Hes 3:2-4; 16:46; 26:61; 16:7, 18; 1Nya 6:3; 1Fal 7:50; Yer 52:19; 2Fal 25:15; 2Nya 4:22; Eze 8:11; Law 16:12; Isa 6:6
Leviticus 10:1-6
Kifo Cha Nadabu Na Abihu
1 aNadabu na Abihu, wana wa Aroni, wakachukua vyetezo vyao, wakaweka moto ndani yake na kuongeza uvumba; kisha wakamtolea Bwana moto usio halali, kinyume na agizo la Mungu. 2 bHivyo moto ukaja kutoka kwa uwepo wa Bwana na kuwaramba, nao wakafa mbele za Bwana. 3 cKisha Mose akamwambia Aroni, “Hili ndilo alilonena Bwana wakati aliposema:“ ‘Miongoni mwa wale watakaonikaribia
nitajionyesha kuwa mtakatifu;
machoni pa watu wote
nitaheshimiwa.’ ”
Aroni akanyamaza.
4 dMose akawaita Mishaeli na Elisafani, wana wa Uzieli mjomba wake Aroni, akawaambia, “Njooni hapa. Ondoeni miili ya binamu zenu mbele ya mahali patakatifu, mkaipeleke nje ya kambi.” 5 eHivyo wakaja na kuwaondoa, wakiwa bado wamevalia makoti yao ya ibada, wakawapeleka nje ya kambi, kama Mose alivyoamuru.
6Ndipo Mose akamwambia Aroni pamoja na wanawe, Eleazari na Ithamari, “Msifunue vichwa vyenu wala msirarue mavazi yenu, la sivyo mtakufa na Bwana ataikasirikia jumuiya nzima. Lakini ndugu zenu, nyumba yote ya Israeli, wanaweza kuwaombolezea wale ambao Bwana amewaangamiza kwa moto.
Copyright information for
SwhNEN