‏ Judges 9:8-15

8Siku moja miti ilitoka ili kwenda kujitawazia mfalme. Ikauambia mzeituni, ‘Wewe uwe mfalme wetu.’

9“Lakini mzeituni ukaijibu, ‘Je, niache kutoa mafuta yangu ambayo kwake miungu na wanadamu huheshimiwa, ili nikawe juu ya miti?’

10“Kisha miti ikauambia mtini, ‘Njoo na uwe mfalme wetu!’

11“Lakini mtini ukaijibu, ‘Je, niache kutoa matunda yangu mazuri na matamu, ili niende nikawe juu ya miti?’

12“Ndipo miti ikauambia mzabibu, ‘Njoo na uwe mfalme wetu.’

13 a“Lakini mzabibu ukaijibu, ‘Je, niache kutoa divai yangu inayofurahisha miungu na wanadamu ili nikawe juu ya miti?’

14“Mwishoni miti yote ikauambia mti wa miiba, ‘Njoo na uwe mfalme wetu.’

15 b“Nao mti wa miiba ukaijibu, ‘Kama kweli mnataka niwe mfalme wenu, basi njooni mpate kupumzika chini ya kivuli changu. Lakini kama sivyo, moto na utoke kwenye mti wa miiba ukateketeze mierezi ya Lebanoni!’

Copyright information for SwhNEN