Judges 2:11-15
11 aKwa hiyo Waisraeli wakatenda maovu machoni pa Bwana na kuwatumikia Mabaali. 12 bWakamwacha Bwana, Mungu wa baba zao, aliyekuwa amewatoa katika nchi ya Misri. Wakaifuata na kuiabudu miungu mbalimbali ya mataifa yanayowazunguka. Wakamkasirisha Bwana, 13 ckwa sababu walimwacha na kutumikia Baali na Maashtorethi. 14 dHivyo hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia mikononi mwa wavamizi waliowateka nyara. Akawauza katika mikono ya adui zao pande zote, hivyo hawakuweza tena kuwazuia adui zao. 15 ePopote Israeli walipotoka kwenda kupigana, mkono wa Bwana ulikuwa kinyume nao ili kuwashinda, kama vile alivyokuwa amewaapia. Nao wakawa katika taabu kubwa.
Copyright information for
SwhNEN