‏ Joshua 19:1-9

Mgawo Kwa Simeoni

1 aKura ya pili ikaangukia kabila la Simeoni, ukoo kwa ukoo. Urithi wao ulikuwa ndani ya eneo la Yuda. 2 bUlijumuisha:

Beer-Sheba (au Sheba), Molada,
3 cHasar-Shuali, Bala, Esemu, 4Eltoladi, Bethuli, Horma, 5Siklagi, Beth-Markabothi, Hasar-Susa, 6Beth-Lebaothi na Sharuheni; hii ilikuwa miji kumi na mitatu pamoja na vijiji vyake.
7Pia Aini, Rimoni, Etheri, na Ashani; hii ilikuwa miji minne na vijiji vyake, 8pamoja na vijiji vyote vinavyoizunguka miji hii mpaka Baalath-Beeri (ambayo ndiyo Rama iliyo katika Negebu).
Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Simeoni ukoo kwa ukoo.
9 dUrithi wa Wasimeoni ulitolewa kutoka fungu la Yuda, kwa kuwa fungu la Yuda lilikuwa kubwa kuliko walivyohitaji. Hivyo kabila la Simeoni lilipewa urithi wao ndani ya eneo la Yuda.

Copyright information for SwhNEN