‏ Joshua 12:2-5

2 aSihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni.

Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ilijumlisha nusu ya Gileadi.
3 bPia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi
Yaani Bahari ya Galilaya.
hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi
Yaani Bahari Mfu.
), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya materemko ya Pisga.

4 eNayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei.

5 fNaye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa watu wa Geshuri, na watu wa Maaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni.

Copyright information for SwhNEN