Jonah 2:3-5
3 aUlinitupa kwenye kilindi,ndani kabisa ya moyo wa bahari,
mikondo ya maji ilinizunguka,
mawimbi yako yote na viwimbi
vilipita juu yangu.
4 bNikasema, ‘Nimefukuziwa
mbali na uso wako,
hata hivyo nitatazama tena
kuelekea Hekalu lako takatifu.’
5 cMaji yaliyonimeza yalinitisha,
kilindi kilinizunguka;
mwani ▼
▼Mwani hapa maana yake ni magugu yaotayo kwenye sakafu ya kilindi cha bahari.
ulijisokota kichwani pangu.
Copyright information for
SwhNEN