‏ John 9:7-11

7 aKisha akamwambia, “Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu.” (Siloamu maana yake ni aliyetumwa.) Ndipo yule kipofu akaenda, akanawa, naye akarudi akiwa anaona.

8 bMajirani zake na wale wote waliokuwa wamemwona hapo awali akiombaomba wakaanza kuuliza, “Je, huyu si yule aliyekuwa akiketi akiombaomba?” 9Wengine wakasema, “Ndiye.”

Wengine wakasema, “Siye, bali wamefanana.”

Lakini yeye akawaambia, “Mimi ndiye.”

10Wakamuuliza, “Basi macho yako yalifumbuliwaje?”

11 cYeye akawajibu, “Yule mtu aitwaye Yesu alitengeneza tope, akanipaka machoni mwangu, naye akaniambia nenda ukanawe katika Bwawa la Siloamu, ndipo nikanawa nami nikapata kuona!”

Copyright information for SwhNEN