‏ John 19:34-37

34 aBadala yake mmoja wa wale askari akamchoma mkuki ubavuni na mara pakatoka damu na maji. 35 bMtu aliyeona mambo hayo ndiye alitoa ushuhuda, nao ushuhuda wake ni kweli. Anajua kuwa anasema kweli, naye anashuhudia ili pia nanyi mpate kuamini. 36 cKwa maana mambo haya yalitukia ili Maandiko yapate kutimia, yale yasemayo, “Hakuna hata mfupa wake mmoja utakaovunjwa.” 37 dTena Andiko lingine lasema, “Watamtazama yeye waliyemchoma.”

Copyright information for SwhNEN