John 18:28-33
Yesu Apelekwa Kwa Pilato
(Mathayo 27:1-2, 11-14; Marko 15:1-5; Luka 23:1-5)
28 aNdipo Wayahudi wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa na kumpeleka kwenye jumba la kifalme la mtawala wa Kirumi. ▼▼Jumba la mfalme la mtawala wa Kirumi lilikuwa linaitwa Praitorio.
Wakati huo ilikuwa ni alfajiri, ili kuepuka kuwa najisi kwa taratibu za ibada, Wayahudi hawakuingia ndani kwa sababu ya sheria za Kiyahudi. Wangehesabiwa kuwa najisi kama wangeingia nyumbani mwa mtu asiye Myahudi na wasingeruhusiwa kushiriki katika Sikukuu ya Pasaka. 29Hivyo Pilato akatoka nje walikokuwa akawauliza, “Mmeleta mashtaka gani kumhusu mtu huyu?” 30Wao wakamjibu, “Kama huyu mtu hakuwa mhalifu tusingemleta kwako.”
31Pilato akawaambia, “Basi mchukueni ninyi mkamhukumu kwa kufuata sheria zenu.”
Wayahudi wakamjibu, “Sisi haturuhusiwi kutoa hukumu ya kifo kwa mtu yeyote.” 32 cWalisema hivyo ili yale maneno aliyosema Yesu kuhusu kifo atakachokufa yapate kutimia.
33 dKwa hiyo Pilato akaingia ndani ya jumba la kifalme, akamwita Yesu, akamuuliza, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?”
Copyright information for
SwhNEN