John 18:25-27
Petro Amkana Yesu Tena
(Mathayo 26:71-75; Marko 14:69-72; Luka 22:58-62)
25 aWakati huo Simoni Petro alikuwa amesimama akiota moto. Baadhi ya wale waliokuwepo wakamuuliza, “Je, wewe si mmoja wa wanafunzi wake?”Petro akakana, akasema, “Sio mimi.”
26 bMmoja wa watumishi wa kuhani mkuu, ndugu yake yule mtu ambaye Petro alikuwa amemkata sikio, akamuuliza, “Je, mimi sikukuona kule bustanini ukiwa na Yesu?” 27 cKwa mara nyingine tena Petro akakana, naye jogoo akawika wakati huo huo.
Copyright information for
SwhNEN