‏ John 11:45-53

Shauri La Kumuua Yesu

(Mathayo 26:1-5; Marko 14:1-2; Luka 22:1-2)

45 aHivyo Wayahudi wengi waliokuwa wamekuja kumfariji Maria, walipoona yale Yesu aliyoyatenda wakamwamini. 46Lakini baadhi yao wakaenda kwa Mafarisayo na kuwaambia mambo Yesu aliyoyafanya. 47 bKwa hiyo viongozi wa makuhani na Mafarisayo wakaita mkutano wa baraza.

Wakaulizana, “Tufanyeje? Huyu mtu anafanya ishara nyingi.
48Kama tukimwacha aendelee hivi, kila mtu atamwamini, nao Warumi watakuja na kupaharibu mahali petu patakatifu na taifa letu.”

49 cMmoja wao aliyeitwa Kayafa, ambaye alikuwa kuhani mkuu mwaka huo, akasema, “Ninyi hamjui kitu chochote! 50 dHamjui kwamba ni afadhali mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, kuliko taifa lote liangamie?”

51 eHakusema haya kutokana na mawazo yake mwenyewe bali kama kuhani mkuu mwaka huo, alitabiri kuwa Yesu angelikufa kwa ajili ya taifa la Wayahudi, 52 fwala si kwa ajili ya taifa hilo pekee, bali pia kwa ajili ya watoto wa Mungu waliotawanyika, ili kuwaleta pamoja na kuwafanya wawe wamoja. 53 gHivyo tangu siku hiyo wakawa wanafanya mipango ili wamuue Yesu.

Copyright information for SwhNEN