‏ Joel 3:9-12

9 aTangazeni hili miongoni mwa mataifa:
Jiandaeni kwa vita!
Amsha askari!
Wanaume wote wapiganaji
wasogee karibu na kushambulia.
10 bMajembe yenu yafueni yawe panga
na miundu yenu ya kukatia iwe mikuki.
Aliye dhaifu na aseme,
“Mimi nina nguvu!”
11 cNjooni haraka, ninyi mataifa yote kutoka pande zote,
kusanyikeni huko.

Shusha wapiganaji wako, Ee Bwana!

12 d“Mataifa na yaamshwe;
na yasonge mbele kuelekea Bonde la Yehoshafati,
kwa kuwa nitaketi mahali pale
kuhukumu mataifa yote yaliyoko kila upande.
Copyright information for SwhNEN