Joel 2:7-8
7 aWanashambulia kama wapiganaji wa vita;
wanapanda kuta kama askari.
Wote wanatembea katika safu,
hawapotoshi safu zao.
8Hakuna anayemsukuma mwenzake;
kila mmoja anakwenda mbele moja kwa moja.
Wanapita katika vizuizi
bila kuharibu safu zao.
Copyright information for
SwhNEN