Job 34:20-25
20 aWanakufa ghafula, usiku wa manane;watu wanatikiswa nao hupita;
wenye nguvu huondolewa
bila mkono wa mwanadamu.
21 b“Macho yake yanazitazama njia za wanadamu;
anaona kila hatua yao.
22 cHakuna mahali penye giza nene, wala uvuli mkubwa,
ambapo watenda mabaya wanaweza kujificha.
23 dMungu hana haja ya kumchunguza mtu sana,
ili apate kuja mbele zake kwa hukumu.
24 eBila kuuliza huwapondaponda wenye nguvu nyingi
na kuwaweka wengine mahali pao.
25 fKwa sababu huyaangalia matendo yao yote,
huwaondoa usiku, nao wakaangamia.
Copyright information for
SwhNEN