Job 18:11-18
11 aVitisho vimemtia hofu kila upande,na adui zake humwandama kila hatua.
12 bJanga linamwonea shauku;
maafa yako tayari kwa ajili yake aangukapo.
13 cNayo yatakula sehemu ya ngozi yake;
mzaliwa wa kwanza wa mauti atakula maungo yake.
14 dAtangʼolewa kutoka usalama wa hema lake,
na kupelekwa kwa mfalme wa vitisho.
15 eMoto utakaa katika hema lake;
moto wa kiberiti utamwagwa juu ya makao yake.
16 fMizizi yake chini itakauka
na matawi yake juu yatanyauka.
17 gKumbukumbu lake litatoweka katika dunia,
wala hatakuwa na jina katika nchi.
18 hAmeondolewa nuruni na kusukumiwa gizani,
naye amefukuzwa mbali atoke duniani.
Copyright information for
SwhNEN